Kijiji cha Mlangarini kipo upande wa kusini mashariki mwa
mji Jiji la Arusha kiasi umbali wa kilometa 15 kutoka mnara wa saa kufuata
barabara ya old Arusha Moshi baada ya kupita shamba la Maua la Dekker Bruis na
Tanzania Flowers.
Kijiji cha Mlangarini kina huduma zote muhimu za kijamii
ikiwepo sekondari ya kutwa na boarding yenye kidata cha kwanza hadi sita.
Vilevile kijiji kina Dispensary ya Serikali pamoja na dispensary binafsi.
Huduma za umeme, maji safi ya bomba pamoja na maji ya kumwagilia vyote
vinapatikana.
Gharama ya nauli kutoka mjini Arusha hadi kijijini
Mlangarini ni shilingi elfu 1000 tu na usafiri wa daladala unapatikana kuanzia
asubuhi hadi saa za usiku.
Ardhi ya kijiji cha mlangarini inafaa kwa shughuli za kilimo
cha mbogamboga ufugaji na makazi.
Mashamba ya viwanja tunavyouza katika kijiji cha Mlangarini
Shamba lenye ukubwa wa hekari mbili linauzwa. Shamba hili lipo katika
kitongoji cha majengo kijijini Mlangarini umbali wa mita 300 kutoka
barabara kuu ya Arusha Nduruma na kuna barabara ya gari hadi katika
eneo. Shamba hili linafaa kwa kulima na makazi kwani lina mfereji wa
maji ya kumwagilia. Vilevile nguzo za umeme ziko umbali wa mita 100
kutoka shamba umbali ambao ni sawa na nguzo mbili tu
Shamba na kiwanja chenye ukubwa wa nusu heka linauzwa katika kijiji cha
Mlangarini kitongoji cha Bondeni. Shamba hili linafikika kwa barabara
ya gari pia lina mfereji wa maji ya kumwagilia. Umeme uko umbali wa
mwita mia kutoka katika eneo hili.